Kumetolewa madai ya kuvutia kuhusiana na simu hiyo inayosemekana kuundwa kwa teknolojia ya hali ya juu.
Sony Xperia Z5 inadaiwa kutumia betri lenye uwezo mkubwa ambalo halijawahi kutumika katika simu nyingine yoyote.
Sony Xperia Z5 itaendeshwa kwa mfumo wa Snapdragon 820 wa 64 bit, na kutumia betri lenye nguvu ya 4500 mAh.
Simu hiyo pia itakuwa na RAM ya 4 GB, HDR, kamera ya nyumba yenye ubora wa 21 MP na skrini ya QHD.
Ingawa maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na ukubwa wa skrini yake, Sony Xperia Z5 inatarajiwa kuongezwa ukubwa na kuwa na nafasi ya USB-C.