Header ads

Header ads
» » Maelezo yanayohusu simu mpya ya Samsung Galaxy Note 5 yavujishwa mtandaoni


 

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Samsung kutoka Korea Kusini, ilikuwa imejiandaa kutambulisha rasmi simu yake mpya aina ya Galaxy Note 5 mwishoni mwa mwaka huu.
Wapenzi wa teknolojia waliokuwa wakisubiria kwa hamu na ghamu walipata fursa ya kuitambua simu hiyo baada ya maelezo yake kuvujishwa mtandaoni.
Kwa mujibu wa maelezo hayo, Samsung Galaxy Note 5 inasemekana kuwa na skrini kubwa ya inchi 5.67 yenye ubora wa QHD Super AMOLED.
Samsung Galaxy Note 5 pia inasemekana kutumia betri lenye nguvu ya 4100 mAh na kuendeshwa kwa mfumo wa Exynos 7422 SoC.
Simu hiyo inatarajiwa kuzinduliwa katika aina tatu tofauti zenye hifadhi ya 32 GB, 64 GB na 128 GB.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post