
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameukejeli uamuzi wa Marekani kuhalalisha ndoa za mashoga katika majimbo yote 50 kwa kuahidi kusafiri hadi White House na kumchumbia Barack Obama.
Wakati wa mahojaino ya kila wiki na kituo cha redio cha taifa, rais wa Zimbabwe alitania kwamba amepanga kwenda Washington DC kupiga goti moja na kuomba kumchumbia Rais Barack Obama wa Marekani. Mugabe, ambaye anajulikana kwa kupinga vikali
mahusiano ya jinsia moja, alikuwa akijibu kuhusiana na marekebisho ya kifungu cha 14 cha Marekani. Katiba inawahakikishia mashoga na wasagaji kuwa na haki sawa kuoana kama walivyo watu wengine.
Akizungumzia hilo siku ya Jumamosi, Mugabe alisema: “Nimeshahitimisha – kuwa tangu Rais Obama aidhinishe ndoa za jinsia moja, kutetea watu mashoga na kufurahia kukubalika –kama vile ni jambo la lazima, nitasafiri hadi Washington, DC, kumchumbia.
Chanzo: Taarifa News