Header ads

Header ads
» » Hiki Ndicho Diamond Platnumz Alichosema Kuhusu Tuzo za Kilimanjaro Music Awards

 
“Well Nimekuwa nikipokea maswali na Comment nyingi eti kwanini sitangazi vipengele vyangu vya Tunzo watu wanipigie kura...tafadhali naomba mniskilize kwa umakini: Ikiwa MOE MUSIC hakuonekana ni Mmoja ya Mwanamuziki bora Chipukizi.. NDAGUSHIMA ya Ommy Dimpoz haikuonekana inafaa kugombe kama Moja ya Video bora..YAMOTO BAND licha ya kuvuma na kujaza kila show ya kila pembe ya Tanzania ila Mwisho wa Siku wameambulia Category Mbili tu Unafkiri mimi nina haja gani ya Kuomba kura???? Hivi kuna Nyimbo zimependwa na kuvuma kama NITAJUTA ama NISEME ya YAMOTO BAND Tanzania?? Eti mwisho wa siku hazikustahili kuwa nyimbo bora, watoto wa watu licha ya Juhudi zote eti wameambulia Category Mbili... Hivi kweli Tunankuza Mziki wetu au Tunaua??? Kuwa na Categories 10 na Kuongoza kwa Vipengele vingi hakunifanyi eti nifurahie Wengine wanapoumizwa...kwani Kwangu mimi sifanyi mziki ili Nifaidike bali nafanya ili Taifa langu na Tasnia yangu izidi kufika mbali na iheshimike... I have been to this Industry zaidi ya Miaka 5 so panapo NAMNA Napajuaga mapema na Ndiomaana sipotezi muda wangu kuomba kura... Wakiona kuna mahala nilistahili watatoa wakiona sijastahili ni haki yangu kutopewa... Coz mwisho wa siku utapigisha watu kura halaf tunzo pia msipewe uonekane ilishindwa kiuhalali kumbe fitna.” 

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post