Iceland imezua hisia kali wakati wa
ufunguzi wa maonyesho ya usanii katika mji wa Venice nchini Italy baada
ya kulibadilisha kanisa ambalo lilikuwa halitumiki kuwa msikiti.
Kwa
jina 'La Moschea' msikiti huo unatokana na jengo la santa Maria della
Misericordia,kanisa moja la kikatholiki ambalo lilikodishwa na Iceland
na mwenyewe.Na ili kuonyesha uvumilivu wa kidini waislamu wengi walijitokeza kuomba katika jumba hilo kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wakiwa wamewacha viatu nje ya lango la jumba hilo,waumini hao walielekea Mecca na kusujudu huku wageni wakiendelea na ziara zao za za utalii katika jumba hilo.
Uwekaji wa msikiti huo ulifanywa na msanii mmoja wa Switzerland Christoph Buechel kwa lengo la kuvutia hisia kutokana na kutokuwepo kwa hata msikiti mmoja katika mji wa kihistoria wa Venice--mji ulio na uhusiano wa kihistoria na ulimwengu wa kiislamu.
Lakini mamlaka ya mji huo imeonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo ikisema kuwa jengo hilo lina hatari ya kushambuliwa na wale wanaopinga Uislamu ama Waislamu wenye itikadi kali.
Rais wa jimbo la Veneto Luca Zaia ametaja hatua hiyo kama uchochezi.