Header ads

Header ads
» » Hawa Ndio Washindi Wa Tuzo Za Watu 2015 #‎TuzozaWatu2015‬


Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili. 

D’Jaro alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.
“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5. 

“Lakini inakushtua kwa njia nzuri kwamba kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa ufanyie kazi zaidi. Lakini pia kura zinamata, inachangia sehemu zote, inawezakana ubora wa kipindi na kura pia. 
Lakini all in all mimi nampongeza sana D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto pia, inatupa nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya kazi kwenye biashara yetu vizuri.”
Hii ni orodha kamili ya washindi

Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM

Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso – TBC FM

Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim Kikeke – BBC Swahili

Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi – EATV

Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com

Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana

Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi

Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu

Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD

Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee

Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba

Filamu inayopendwa
Kigodoro

Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz 

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post