Header ads

Header ads
» » MSICHANA AMNYONGA MTOTO WA MIAKA 9 KISA SOKSI HUKO MOROGORO

Msichana Judith Chomile (15) amekiri kumnyonga hadi kufa mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Bernard Benderi aliyejulikana kwa jina la Edrini Mafuele baada ya kukorofishana wakiwa nyumbani kwao Kola Hill mjini Morogoro.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema msichana huyo alimnyonga mtoto huyo siku ya Jumatano baada ya kutokea mabishano kati ya marehemu na mtuhumiwa.
Amesema marehemu alikuwa akimtuhumu dada yake kumuibia soksi za shule huku akimrushia maneno ya kejeli ndipo mtuhumiwa akachukua uamuzi wa kumsukuma marehemu.
Amefafanua kuwa baada ya marehemu kudondoka sakafuni mtuhumiwa alimbeba kumpeleka chumbani kisha kumnyonga kwa kutumia kamba ya gauni na kusababisha kifo chake.
Nao wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia tukio hilo wametupia lawama baadhi ya wazazi kuwanyanyasa ndugu zao ambapo wamesema wazazi na walezi wanawajibu wa kuhakikisha wanawalea watoto kwa kuzingatia haki sawa ili kuepusha mauaji na unyanyasaji usiokuwa wa lazima.
 Via>>ITV

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post