Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’
ameeleza kusikitishwa na kitendo cha yule aliempiga picha zile akiwa
stejini akitumbuiza kwani ilikuwa ni bahati mbaya na sio makusudi.
Shilole amesema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani
wakati akitumbuiza Ubelgiji hivi karibuni, kwa sababu ilikuwa bahati
mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.
“Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri […] yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performance, ilitatuka wakati niko kwenye motion .” Alisema Shishi kupitia 255 ya Clouds Fm.
Ameongeza kuwa amesikitishwa na mtu aliyempiga picha hizo na kuamua kuzisambaza mtandaoni bila kujua kuwa itamuumiza yeye kama mwanamke.
“Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.”
Kauli hii ya shilole ameitoa mara baada ya hivi karibuni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kumpa onyo kali staa huyu kwa kitendo kilichotokea.
Kuhusu kama amepokea barua ya kuitwa kujieleza kutoka BASATA, Shishi amesema kuwa hajapokea barua hiyo kwasababu bado yuko Ubelgiji.
WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA
NA VYUO VYA UALIMU MEI 2015/2016
ORODHA YA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA KUJINGA NA MAFUNZO YA UALIMU
AWAMU YA PILI MWAKA WA MASOMO 2014/2015
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi limechagua waombaji 2,543 (Me 1,651
na Ke 892) kujiunga na Mafunzo ya Ualimu
katika Awamu ya Pili ya Mwaka wa Masomo2014/2015. Waombaji 1,968 (Me
1226, Ke 742) wamechaguliwa
kupitia mfumo wa pamoja wa udahili wa wanachuo
(Central Admission System – CAS) na waombaji 575
(Me 425,Ke 150) wamechaguliwa na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi. Majina ya waliochaguliwa
yamewekwa kwenye tovuti ya NACTE
(www.nacte.go.tz) na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi (www.moe.go.tz) na yametumwa
kwa wakuu wote wa vyuo na maafisa
elimu wa mikoa na wilaya.
Waombaji wamechaguliwa kujiunga na vyuo
vya Ualimu vya Butimba, Tabora, Tukuyu
Mpwapwa, Kinampanda, Mhonda, Nachingwea, Singachini na Tandala. Vyuo
vingine ni Tarime
Bustani, Marangu, Morogoro, Klerru naSongea.
Mafunzo ya Ualimu yataanza tarehe 01/06/2015 au la kama ilivyoelezwa
kwenye fomu za maelekezo za chuo husika, hivyo wanachuo wanatakiwa
kuanza kuripoti
vyuoni kuanzia tarehe 28/05/2015. Fomu za
Maelekezo ya Mafunzo (Joining Instructions) yameambatishwa. Pamoja na
maelekezo yaliyopo
kwenye fomu za kila chuo, mwanachuo anatakiwa
kuripoti chuoni akiwa na vyeti halisi vya masomo
na kwa ajili ya taratibu za usajili.
Mwombaji yeyote aliyechaguliwa ambaye chuo
chake si miongoni mwa vyuo vilivyotajwa lakini
ni chuo cha serikali ataweza kuomba uhamisho
kwenye vyuo tajwa kwa kuandika barua au
kupiga simu 0768 614045 la sivyo atajiunga
na masomo mwezi Septemba 2015.
Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni tarehe
25 Mei 2015.
ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA (BOFYA HAPA)
KUPATA JOINING INSTRUCTIONS(BONYEZA HAPA)
IMETOLEWA NA:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE 15/05/2015
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ