Header ads

Header ads
» » TAARIFA KUHUSU SHERIA YA MATUMIZI YA MTANDAO KUTINGA BUNGENI


Na Elvan Stambuli
‘SARAKASI’ za Mkutano wa 19 wa Bunge la 10 zimeanza mjini Dodoma na imeelezwa kuwa ni maalum kwa ajili ya kushughulikia miswada ya sheria ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015) na ya vyombo vya habari ambazo tayari zimetinga bungeni.

Bunge la jamhuli ya muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge, jumla ya miswada sita itawasilishwa bungeni kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa katika hatua zake zote. 

Pamoja na Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, mingine ni Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa Mwaka 2015 (The Access to Information Bill, 2015), Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015 (The Media Services  Bill, 2015) na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 (The Fair Competition Amendment Bill, 2015).   

Miswada mingine ni  Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa Mwaka 2015 (The Electronic Transaction Bill, 2015) na  Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The Natural Gas Bill, 2015). 

Kuja kwa miswada ya habari kunaweza kuwa ‘ukombozi’ kwa wana habari kwani wamekuwa wakiilalamikia serikali, baadhi yao wakidai kuwa sheria zilizopo zinakandamiza na kuwanyima kupata habari. Vikao hivyo vya bunge vitamalizika Aprili Mosi, mwaka huu.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post