Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara
wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya
Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini
unaotekelezwa na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea
kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Baada ya kufika katika eneo hilo wananchi hao walianza kumzomea
wakidai ni “mwizi wa fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow
kelele ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona
anayezomewa ni waziri yupi.
Hata hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo
ambaye yuko ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali
katika eneo hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika
mpango mzima wa mgogoro wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye
akaunti hiyo ya Escrow.
Pamoja na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake
wilayani Kahama ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu
baada ya kuwaahidi umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati
vijijini.