Mbarali. Imeelezwa kuwa makada 10 wa vyama vya CCM na Chadema wameanza kulisaka Jimbo la Mbarali linaloshikiliwa na Mbunge Dickson Kilufi.
Kilufi kutoka CCM amelitumikia jimbo hilo kwa
miaka minne tu, lakini kwa sasa amezungukwa na kundi la wanasiasa,
wafanyabiashara na wasomi wanaoitaka Mbarali.
Duru za kisiasa zinasema kwenye kila chama kuna
makada watano wanaodaiwa kuanza kujipitisha kwa wakazi wa jimbo hilo ili
kuungwa mkono.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo
Mwangomo alisema jana kuwa ofisi yake haijaanza kupokea majina, lakini
anazo taarifa za watu wanaolitaka jimbo hilo.
Alisema CCM haina tatizo kwa yeyote kujitokeza kugombea, lakini siyo kuanza kupiga kampeni.
Mwenyekiti wa Chadema wilayani hapa, Peter
Mwashiti alisema amepokea majina matano ya wenye nia ya kugombea ubunge
katika jimbo hilo.