Header ads

Header ads
» » ZINGATIA HAYA UPATE MAFANIKIO ZAIDI

 kazi inayolipa
MWANADAMU katika maisha yake ya kawaida mafanikio ni ndoto kubwa sana kutokana na malengo mtu aliyojiwekea. Vijana wa kipindi hiki wamekuwa na elimu ya kufanya mambo mbalimbali ili kupata mafanikio.
Pengine hawajui namna ama kupuuzia mambo ambayo yanaweza kuleta mafanikio. Wengine wamekuwa wakitaka mafanikio ya haraka kwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na tamaduni za sehemu mahalia na zaidi kufanya mambo ambayo ni kinyume na Mwenyezi Mungu. Ili upate mafanikio pasipo kutenda yasiyo mpendeza Mungu yakupasa kijana mkristo kufuata yafuatayo ili utimize malengo yako na kufurahia mafanikio yako yaliyo na mwisho mzuri. Mafanikio yoyote yanahitaji bidii kama maandiko yanavyosema kuwa asiye fanya kazi na asile, 2 wathesalonike 3:10. Maandiko hayamaanishi kula tu bali mafanikio yanayopatikana baada ya juhudi hizo. Kijana unatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili ufikie malengo uliyojiwekea ndipo mafanikio yataweza kutokea, ila kufanya kazi kwa bidii yakupasa pia kujiombea ili upate nguvu za kufanya kazi hiyo kwa bidii. Ili Mungu awe anatembea na wewe kwa kila jambo na malengo yako inakupasa kutenda yale aliyoagiza, naye atakusaidia katika kukupa nguvu ya kutimiza malengo yako kama ule usemi usemao Mungu hamtupi mja wake. Kijana anapaswa pia kujali muda wake kwa namna anavyoendesha maisha yake kwani muda ni mali kubwa tena hasa katika kujitafutia maendeleo. Ukidharau muda ni dhahiri kabisa kupoteza baadhi ya majukumu mengine ambayo ulipaswa kufanya kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika maisha yako. Dhibiti ulimi wako sehemu yoyote ambayo upo, kuna msemo unaosema ‘ulimi hutenda’ hivyo ukitumia ulimi wako vizuri una asilimia kubwa ya kupata mazuri sehemu mbalimbali . Ukiwa kazini ni rahisi watu kutamani kuwa na wewe muda wote kwani kinywa chako huneno yaliyo mema wakati wote. Ukisoma 1Petro 3:10 utaona jinsi Mungu anavyotuagiza kutumia ulimi wetu kwa yaliyo mema kwa kulitangaza neno lake “Kwa maana,atakaye kupenda maisha na kuona siku njema,azuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isiseme hila”. Epuka kula na kunywa kupita kiasi, katika mchakato wa kutafuta maendeleo kula na kunywa kupita kiasi kunasababisha kurudisha nyuma maendeleo yako kwani unakuwa unatumia pesa bila sababu za msingi. Mithali 23:21 “ Kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini na utepetevu humvika mtu nguo mbovu,” neno la mungu pia linatuasa kula na kunywa kwa kiasi kwani mlevi na mlafi huishia kwenye umasikini daima mpaka kukosa hata vazi zuri la kuvaa. Chagua marafiki wenye hekima, kwani marafiki nao wana nafasi kubwa katika kutafuta maendeleo yako. Marafiki mwenye hekima watakupa njia mbalimbali za kupata maendeleo. Ukarimu wakati wa kutafuta maendeleo unahitajika kwa hali ya juu ili watu waweze kukuamini na kutamani kufanya na wewe kazi ambazo zinaweza kukupatia kipato kwa ajili ya maendeleo yako. “Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu jinsi alivyosema mwenyewe, ni heri kutoa kuliko kupokea,” Matendo 20:35. Ukitoa Mungu anakupa mara mbili hivyo kijana unatakiwa kuwasaidia wasiojiweza kwa kiasi kile unachokiweza naye Mungu atakurudishia mara mbili ya kile ulichokitoa kwa moyo bila kunung’unika. Jitahidi kutolipa kisasi kwa lolote ambalo umefanyiwa ubaya kwani maandiko yanasema usilipe ubaya kwa ubaya ila ulipe kwa yaliyo mema. Maendeleo yanaendana na kutenda yaliyo mema kwani ukilipa visasi ni ngumu kuishi kwa amani. Warumi 12:17 “ Msimlipie mtu uovu kwa uovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote,”. Yakupasa kutenda yaliyo mema machoni mwa watu ila sio kwa kulipa ubaya kwa ubaya. Kwenda kinyume na maandiko ya Mungu hutufanya kukosa Baraka zake na kurudisha nyuma maendeleo kwa kupoteza muda kujiuliza na kupanga kwa namna gani kisasi chako na kwa gharama yoyote ile kinamfikia aliyekutendea ubaya. Mafanikio ya kitu chochote yakupasa kutenda yampendezayo Mungu ili kuwe na mwisho mzuri tofauti na kutaka mafanikio ya haraka na kuwa na mwisho mbaya.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post