Header ads

Header ads
» » WAAMUZI KUMI NA MOJA TANZANIA KWENYE ORODHA YA FIFA

fifa logo 600x438 FIFA To Suggest Two Winter Kick Off Dates For 2022 World Cup In Qatar

nembo ya shirikisho hilo,iliyo nakshiwa vyema
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa orodha mpya ya waamuzi linaowatambua ,Kwenye orodha hiyo kuna jumla ya waamuzi 18 kutoka Tanzania,miongoni mwa waamuzi hao waamuzi 11 wapya na 7 wa zamani.
Waamuzi wapya wa kati kutoka Tanzania ni Mfaume Ali Nassor kutoka visiwani Zanzibar pamoja na Martin Saanya kutoka Morogoro, pia wamo waamuzi watatu wa kike ambao ni Florentina Zabron ,Jonesia Rukyaa pamoja na Sofia Ismail.
Kwa upande wa waamuzi wasaidizi wanaume ni Frank John Komba na Soud Idd Lila , kwa upande wa wanawake ni Kudura Omary Maurice,Hellen Joseph Mduma,Dalila Jafari Mtwana na Grace Mawala.
Waamuzi wa zamani wa Tanzania kwenye orodha ya FIFA ,kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni Nkongo na Waziri Sheha Waziri,kwa upande wa waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali,Fernand Chacha,John Longino Kanyenye ,Ali Kinduli na Samuel Hudson Mpenzu

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post