Header ads

Header ads
» » TAARIFA KAMILI KUHUSU NDEGE YA RAIS WA CHINA KUHUSISHWA NA WIZI


Rais Xi JinPing wa Uchina alizuru nchini tanzania mwaka uliopita

Inadaiwa kuwa wanunuzi, raia wa Uchina walinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu nchini Tanzania na kuzitorosha kutoka nchini humo katika ndege ya kibinafsi ya raia wa Uchina Xi Jinping,wakati alipozuru bara Afrika.
Kulingana na shirika la ujasusi la mazingira lililo na makao yake mjini London.
Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja tu kabla ya ziara ya rais huyo wa Uchina nchini tanzania mwaka ulioipita ambapo zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili kutokamatwa.

 
Pembe za ndovu
Shirika hilo pia linadai kwamba wajumbe waliokuwa wakiandamana na Rais Xi walinunua viwango vikubwa vya pembe hizo.
Uuzaji wa Pembe za ndovu ulipigwa marufuku mwaka 1989 ili kuwazuia wawindaji haramu kuwaua ndovu.

CHANZO CHA HABARI
BBC

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post