Header ads

Header ads
» » MADHARA YA KUFANYA KAZI KUPITA KIASI NYAKATI ZA USIKU

 
Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la Occupational and Environmental Medicine kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.
Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo wamekuwa wakilala usingizi wa mang'amung'amu.

Moja ya madhara yatokanayo na kufanya kazi usiku ni kuongezeka uzito kupita kiasi
Wataalam hawa wamesema kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya Saratani na uzito mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara ya kiakili pia.

CHANZO CHA HABARI:
BB, jarida la Occupational and Environmental Medicine

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post