Gari la dude muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi.
GARI la
muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na
Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi
linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka
huu.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz
lenye namba za usajiliT 360 BAJ, lilikutwa
likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya Seif
Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSCiliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Inadawa
kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi na kulitambua
gari lake, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo
kumshikilia katika kituo kidogo cha Polisi Mabatini hadi kesho yake
alipodhaminiwa.
Muonekano wa gari hilo kwa nyuma.
Waandishi
wetu walifanya jitihada za kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo,
lakini aliwataka kufuatilia jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema
suala hilo lipo mikononi mwao.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI
Credit GPL