Header ads

Header ads
» » TAARIFA KAMILI KUHUSU MADIWANI 6 KUVULIWA NYADHIFA ZAO BUKOBA




Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera, imewavua nyadhifa zao madiwani sita (6) wa manispaa ya Bukoba na kutangaza kuwa kata zao zipo wazi baada ya kuwatia hatiani kwa kugoma bila sababu kuhudhuria vikao vilivyoitishwa kwa mujibu wa sheria.


Akisoma hukumu katika shauri lililofunguliwa na diwani wa kata ya Kahoro Mheshimiwa Chief Karumuna, hakimu wa mahakama hiyo mheshimiwa Charles Wisso, amesema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kuwa madiwani hao walivunja sheria kwa kutohudhuria vikao vilivyoitishwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Aidha katika hukumu hiyo mahakama imeamuru madiwani hao kulipa gharama zote za kesi na kuagiza kuwa waziri mwenye dhamana ajulishwe kuwa madiwani sita wamepoteza sifa hivyo kata walizokuwa wakiwakilisha zipo wazi, tangu baada ya hukumu hiyo.

Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo iliyochukua takribani saa moja na nusu, hakimu Wisso amesema kuwa mlalamikaji aliwatuhumu madiwani hao kwa kususia vikao kwa maelekezo ya mbunge wa Bukoba Mjini Baalozi Khamis Kagasheki na hivyo kuiomba mahakama itangaze kuwa madiwani hao walikuwa wamepoteza sifa.
Hakimu Wisso pia amesema utetezi wa madiwani hao haukuwa na sababu za msingi za kutohudhuria vikao na hivyo madiwani sita kutiwa hatiani kati ya madiwani nane (8) waliolalamikiwa. 
Madiwani waliopoteza viti vyao, ni pamoja na Yusuph Ngaiza wa kata Kashai, Dauda Karumuna wa kata Ijuganyondo, Deus Mutakyahwa wa kata Nyanga, Samwel Ruhangisa wa kata Kitendaguro, Murungi Kishwabuta na Rabia Badul ambao ni madiwani wa viti maalum.
Chama Cha Mapinduzi CCM kimepoteza madiwani watano (5) huku Chama Cha Wananchi CUF kikipoteza kiti kimoja.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post