Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliyofanywa na Afrobarometer Utafiti ambao uliofanywa mwaka 2016. unadai Watumiaji wa simu Afrika ni wengi kuliko wanaopata maji salama.
Ripoti hiyo inaonyesha
idadi ya watu ambao wanapata huduma ya majisafi, wenye mawasiliano ya simu
za mkononi, umeme na mambao mengine.
Majibu ya ripoti
hiyo yanaonesha watu wanaotumia huduma ya simu za mkononi Africa ni 93% ya
watu wote waliopo Afrika, wakati huohuo watu wanaopata huduma ya
majisafi ni 63%.
Kwenye ripoti hiyo pia inasema
kwamba watu wa Afrika 65% wanapata huduma ya umeme, 54% wanatumia
barabara zinazopitika, na 30% tu ndio wanaoishi kwenye makazi ambayo yana
huduma ya kuhifadhi majitaka (Sewerage)
Chanzo: afrobarometer.org