Simu ya Huawei P8 Lite ilipookoa uhai wa mwanaume wa miaka 41 pale alipovamiwa nje tu ya nyumba yake, Alipigwa risasi ambayo kwa bahati tuu ilipiga kwenye simu yake ya Huawei iliyokuwa kwenye mfuko wa koti lake.
Simu hiyo ya Huawei P8 Lite ilikuwa na ubora wa kutosha kuweza kutoruhusu risasi hiyo kupenya kwa urahisi na kuingia kwenye mwili wake. Risasi ilinasa ndani ya simu.
Simu ya Huawei P8 Lite yenye ukubwa wa inchi 5 inakijumba cha plastiki (housing) na inapatikana kwa takribani Tsh laki 4.
Habari ya tukio hili iliandikwa kwa kujivunia sana huko nchini China. Wakifurahia kuona ubora wa bidhaa zao.
Huawei walimpa zawadi ya simu nyingine Bwana Abrahams baada ya kupata taarifa kuhusu tukio hilo.