Shirika la ndege la Uingereza la British Airways latangaza kuboresha huduma zake kwa kuanza kuwapa abiria wake tembe ya kidijitali ambayo itaweza kupima kiwango cha njaa kwa wasafiri hao .
Kidonge hicho kitaweza kusaidia katika kupanga ratiba ya saa za mlo wakati wa safari ya ndege .
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwa The Telegraph ni kuwa tembe hizo za dijitali ni mojawapo ya mapendekezo ya shirika hilo la ndege la utumizi wa vihisi vya mitandao vitakavyoweza kupima awamu za usingizi za abiria,mapigo ya moyo na pia joto la mwili.
Teknolojia hiyo mpya inalengwa kuboresha uzoefu wa usafiri kwa kusimamia nyakati za kulala za abiria,matumizi ya burudani na pia nyakati za chakula kwa wasafiri.