Header ads

Header ads
» » » Teknolojia ya mawasiliano kuisaidia kukuza Uchumi wa watu wa chini


Matumizi ya teknolojia na mawasiliano yataisaidia Tanzania kuondoa mtu wa kati (dalali) katika biashara hasa kwa wajasiriamali wadogo sana, wadogo na wakati kwa sababu muuzaji na mnunuzi wataweza kuunganishwa kwa kupata taarifa sahihi kuhusu bidhaa husika sokoni.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa mahusiano bora na endelevu katika sekta ya biashara kwa ushirikiano wa Vodacom na shirika la maendeleo ya viwanda vidogo SIDO ambapo amesema mtu wa kati maarufu kama dalali amekuwa akitumia fursa kuwanyonya wafanyabiashara na wakulima hao kutokana na wao kutokuwa na taarifa sahihi za soko, hivyo mahusiano hayo ya Vodacom, Sido na wajasiriamali yatawezesha mjasiriamali kupata taarifa sahihi pale alipo kupitia simu yake ya mkononi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO), amesema teknolojia na mawasiliano itawafaa wajasiriamali kuweza kuunganisha shughuli zao na kuanzisha viwanda, huku akisisitizia pia elimu ya biashara kwa wajasiriamali ili waweze kuzalisha kibiashara, pamoja na kujua namna ya kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zao zinazokidhi ubora.
Mfumo wa mahusiano bora na endelevu uliozinduliwa na vodacom leo umelenga sekta ya biashara ili kurahisisha mfumo wa mawasiliano katika biashara kufuatia wajasiriamali kutawanyika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kuwawezesha kuuza wakiwa umbali mrefu, kubaini masoko pamoja na bei ya bidhaa husika. 

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post