Siku ya August 11, 2016 Gazeti la Bangladesh Daily Star liliripoti kuwa Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Simu ya Bangladeshi iliamuru waendeshaji wa mitambo ya mitandao ya Internet ya kimataifa kufungia tovuti za habari zipatazo 35.
Hakuna maelezo zaidi yaliyojitokeza kuhusu kufungiwa huko mpaka sasa, lakini orodha ya tovuti hizo ni ndefu na inajumuisha tovuti zinazowakilisha maeneo muhimu ndani ya nchi hasa katika hali ya kisiasa ya sasa ya nchini.
Mpango wa kuzima internet ulitangazwa Agosti 1 na kuwasilishwa kama mkakati wa kiusalama. Hili linafanyika kufuatia uvamizi wa kikatili uliofanyika mapema Julai katika enei la kuokea mikate la Holey Artisan, ambapo mateka wapatao 20 waliuawakama sehemu ya shambulio la kigaidi lililokuja katika kipindi ambacho vurugu zinaongezeka nchini .
Pamoja na mtandao wa intaneti huduma nyingine pia zilikatwa. Makampuni ya uendeshaji wa simu za mikononi yaliripotiwa kupimwa uwezo wao kuzima miito ya sauti na ISPs pia waliambiwa wafungie baadhi ya tovuti. Haijaeleweka vizuri kama tovuti hizi ndio zile zile zilizoamriwa kufungiwa hapo Agosti 4.
Mwenyekiti wa Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Simu nchini Bangladeshi (BTRC), Shahjahan Mahmood, kuwa hili zoezi lilikuwa la kwanza kati ya mfululizo wa kuzima kwa muda kwa mitandao ya internet, anasema “Kama sehemu ya zoezi linaloendelea, aina zote za mitandao ya internet itasimamishwa kwa kipindi kifupi kwa muda wowote na mahali popote hapa nchini,”
Ahsan Habib Khan, makamu mwenyekiti wa BTRC aliongezea kuzimwa huko kwa mitandao hiyo mara nyingi itakuwa inafanyika wakati wa usiku na siku za mapumziko.
Wananchi wanapambana kuona jinsi kuzimwa huko kwa mitandao kutakavyokuwa na matokeo chanya katika usalama wao, lakini changamoto zimeonesha kukwama kwa mkakati huo. Wananchi wa Bangladeshi wameeleza masikitiko yao na hasira zao kupitia mitandao ya kijamii kwa mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook