Kutokana na ukuaji wa Teknolojia pamoja
na kasi kubwa iliyopo Duniani kwenye soko la Ushindani na Ubunifu, kila
siku tunaona ubunifu mkubwa sana ukichukua vichwa vya habari kubwa
Duniani !!
Kulikuwa na magari yanayotumia mafuta,
zimekuja gari zinazotumia na nishati nyingine ikiwemo gari za umeme..
ikaja sasa badala ya kupokeza muda kuchaji gari, Uingereza
wakaitambulisha teknolojia ya barabara zinazochaji gari za umeme… hiyo
ni mfano tu wa Taarifa za kukua kwa teknolojia kwenye kasi kubwa sana
Duniani.
Hapa nimekusogezea Daraja la kioo toka China Daraja
limekamilika na lina urefu wa kama Mita 300 hivi ambazo kwa hesabu ya
kawaida ni urefu wa viwanja vitatu vya mpira, yani kutoka goli mpaka
goli alafu viwanja viwe vitatuUnaambiwa kwamba upana wa kioo kilichotumika kwenye huu ujenzi kina kama Milimita 24 ambazo ni kama mara 25 ya upana wa kioo cha kawaida, kwa hiyo hakuna shaka kuhusu uimara na usalama wa Daraja lenyewe
Daraja hilo limejengwa kuunganisha sehemu ambayo ni juu ya Milima kwenye Hifadhi ya Shiniuzhai Park, ambayo iko kwenye Jimbo la Hunan, Kusini mwa China.
Sehemu ya chini ambayo unaikanyaga unapovuka Daraja imetengenezwa kwa kioo kitupu
Kama una tatizo la kizunguzungu hapouwezi pita
Chanzao: indiatimes.com