Mahakama moja ya Marekani imeamuru kampuni ya Apple kusaidia idara ya upelelezi ya FBI ili kufikia data za simu ya mshukiwa wa ugaidi.
FBI imekuwa ikipeleleza washukiwa wa ugaidi Syed Farook na mkewe Tashfeen Malik wanaodaiwa kutekeleza mashambulizi tarehe 2 Desemba mwaka jana katika mji wa San Bernardino, California.
Washukiwa hao wawili wanadaiwa kuua watu 14 kwa kuwafyatulia risasi kabla ya kuuawa na polisi.
Jaji wa mahakama hiyo Sheri Pym alitaarifu kampuni ya Apple baada ya FBI kushindwa kufikia data za simu hiyo aina ya iPhone iliyokuwa imefungwa na nywila ya siri.
Kwa kawaida idara ya FBI ina utaratibu wa kuchunguza kwa undani vifaa vyote binafsi vilivyokuwa vikitumiwa na mshukiwa yeyote anayefanyiwa upelelezi.
SOURCE: CNN NEWS
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM