Takriban maafisa 1,000 wa serikali za mitaa,viongozi wa dini na walimu wakuu ikiwa ni pamoja na wanafunzi watapewa mafunzo ya jinsi ya kutumia huduma hiyo ya Android iliyo bure kwa muda wa miezi sita.
Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa kati ya wasichana 3 chini ya umri wa 18 moja wao amepata unyanyasaji wa kijinsia.
Programu hiyo ya Android inajulikana kama Equality Effect itaanzishwa kutumika katika miji mikubwa nchini Kenya.
Programu hiyo itaunganisha muathirika wa ubakaji na polisi pamoja na mahali kitendo hicho kitakapotekelezwa na itarahisiha ufuatiliaji wa kesi hiyo.
Tayari polisi 700 wamepokea mafunzo ya jinsi ya kutumia programu hiyo na jinsi ya kutambua wabakaji hao.