Header ads

Header ads
» » Matumizi mabovu ya Intaneti yanatengeneza Kizazi Kililichopungukiwa Raha

 
Watoto wa siku hizi wana mtazamo mdogo wa ndani kuhusu uwezo wao na wanakabiliwa na hisia za upweke.
Hili limebainika na huduma ya kushughulikia matatizo ya watoto ya
ChildLine , iliyobaini ongezeko la malalamiko ya kukosa raha ya maisha, huku wakihusisha ongezeko hilo na matumizi ya intaneti huko nchini Uingereza.
Jarida la theNextWeb linamnukuu meneja wa huduma ya ChlidLine, Mairead Monds akisema, “Ni wazi kwamba msukumo wa kuwiana na marafiki pamoja na kuwa na maisha bora machoni mwa watu unawapunguzia raha vijana wengi kila siku.” Watoto wanajikuta wakilazimika kuiga maisha ya watu na kuhangaika kuonesha maisha yao jinsi wao wanavyotaka kujionesha, ambayo ni tofauti kabisa maisha yao halisi. Huko mtandaoni wanakumbana na matatizo mengi zaidi, ikiwemo urafiki usio wa ukweli. Watoto wameonekana kuhamasika kiurafiki na idadi ya “like” wanazozipata kutoka kwa wengine na kufikia kulinganisha idadi hiyo na nguvu waliokuwa nayo ya kupendwa.
 

Tatizo Ni Kujithaminisha
           
Does your child need a detox from the Internet?
                                     Picha na ahchealthenews.com/
Kadri wakati unavyozidi kuenda, intaneti inazidi kuchukua sehemu kubwa ya maisha yetu. Watoto wako kwenye hali ya hatari zaidi ya kudhurika na intaneti. Ukilinganisha, watu wazima hawako hatarini sana kwa sababu wanaweza kukumbuka maisha yalivyokuwa bila intaneti kama ilivyotanda sasa hivi. Zamani ukipata tatizo, unaweza kulikimbia na kusahau ila katika zama hizi za kisasa, tatizo likishaingia mtandaoni inakuwa vigumu sana kulikimbia na inahitaji nguvu za ziada za binafsi kujitetea au kuweka msimamo dhidi ya matatizo hayo.

Taarifa ya theNextWeb inaelezea kwamba tayari stadi nyingi zinafanyika kulinganisha hali ya furaha na matumizi ya intaneti, au kuwa karibu zaidi na mtandao. Kwa mfano, mwaka 1998, Robert Kraut, mtafiti wa Chuo cha Carneige Mellon alikuta kadri watu wanavyotumia mtandao wa intaneti,
nayo furaha yao inapungua. Kuna stadi nyingine ilifikia kusema kwamba huenda Facebook ikachangia kuvunjika kwa mahusiano kwa kuongeza hisia za wivu.
Kuna tatizo kubwa zaidi kwenye mitandao ya jamii ambalo wanasaikolojia wanaliita Social Comparison, yani kujilinganisha ama kujithamanisha kama una akili, uwezo au unavutia zaidi ya watu wengine kwa kuuliza maswali au kutafuta kukubalika na watu wengine. Suala hili limekuwa sana pamoja na teknolojia ya mtandao ya sasa. Makala hii inaenda zaidi kufananisha tatizo hili na njaa au kiu kwani mtu anajisikia kukosa kitu flani asipoangalia ukurasa wake wa instagram kwa muda mrefu.
Mwandishi wa makala anaeleza kwamba kujithamanisha ni kitu cha kawaidia cha kisaikolojia kinachofanywa na watu kwa madhumuni ya kujipa imani na kujiendeleza. Ila suala hili kwa vijana wanaokuwa na kutafuta kujua wao ni nani kwenye hii dunia ni changamoto, kutokana na hali ya mitandao ilivyofikia hivi sasa. Kama watu wazima, tumejifunza kwa muda mrefu jinsi ya kukakamaa na kujikaza na kufanya mambo ya msingi kukabiliana na kujithaminisha ila kwa vijana wadogo, unaweza kuona ni jinsi gani changamoto hii inavyoweza kuwasumbua.
 

Vijana Wanatambua hili
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa ikiwamo jarida la Elle , ipo mifano ya vijana wadogo wanaoonesha kuelewa jinsi mitandao ya kijamii yanavyowaathiri na kuweza kufanya mapinduzi. Kuna stadi iliyofanyika na Girl Scouts (Marekani) na kugundua kwamba asilimia 74 ya wasichana walikubali kwamba wenzao wanaonekana kuwa na mvuto bora zaidi kwenye mitandao zaidi ya walivyo katika hali halisi. Pia, wapo vijana wanaoacha kutumia mitandao na kupaisha maoni yao juu ya waliyofanya yasio ya ukweli kwenye mitandao. Wapo vijana ambao wanatumia akaunti tofauti kwenye mitandao, moja ikiwa ya kuvuna mashabiki (“followers”) na nyingine wakizitumia kuonesha hali halisi walizokuwa nazo.

                   
  • Kijana Essena O’Neill wa Australia aliachana na Instagram huku akiwaambia mashabiki wake 612,000 jinsi alivyotumia akaunti hiyo kibiashara, huku akionesha maisha yasiyo yake kama wengi walivyodhania.

Maswala ya ubinadamu na teknolojia ya sasa yanaweza kuwa magumu. Si watoto, si vijana wadogo na hata watu wazima wanaweza kukwepa madhara yake bila msaada au nguvu ya ziada. Ni jambo la muhimu kuwa na mjadala juu ya matumizi ya mitandao. Vijana wadogo wanahitaji watu wa kuwapa dira kuhusu utumiaji mzuri wa mtandao. Je unafanya hili kwenye jamii yako?





Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post