Mzee huyo aliumwa mguuni na papa wakati alipokuwa akizunguka na boti baharini siku ya Ijumaa mwendo wa saa tano asubuhi, katika eneo la umbali wa kilomita 300 kutoka pwani ya Sydney.
Kwa bahati nzuri mzee huyo aliokolewa na wahudumu waliowasili na Ambulansi katika pwani hiyo, na baadaye akasafirishwa kwa helikopta hadi katika hospitali ya karibu.
Visa vya mashambulizi ya papa vimekuwa vikitokea nchini Australia ambapo watu wawili wamepoteza maisha huku wengine wengi wakijeruhiwa ndani ya miezi 12 ya hivi karibuni.
Serikali ya Australia imetangaza mpango wa kutaka kuweka vizuizi vya nyavu katika pwani za Sydney, ingawa wataalamu wa hifadhi za mazingira wameonya kwamba hatua hiyo huenda ikasababisha viumbe vingine vya baharini kuangamia.