Klabu ya Chelsea inatarajiwa kukata
rufaa dhidi ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa mlinda mlango Thibaut
Courtois katika mchezo uliopigwa jumamosi dhidi ya Swansea ambao uliisha
kwa droo ya magoli mawili katika uwanj wao wa nyumbani Stamford Bridge.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji huyo mwenye umri wa miaka 23
alitolewa nje dakika ya 52 baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji
Bafetimbi Gomis wa Swansea ambaye alikua anakwenda kushinda ambapo
Swansea walipata penalti kutokana na faulo hiyo.Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kuongelea uamuzi huo baada ya kipute cha mwisho. Rufaa ya Chelsea itasikilizwa na chama cha soka nchini Uingereza FA siku ya jumanne.
Iwapo rufaa hiyo itakataliwa, Courtois ambaye anatarajiwa kufungiwa mchezo mmoja atakosekana katika safari ya kuwakabili washindi wa pili kwenye msimu uliopita Manchester City jumapili ijayo.
ikumbukwe kwamba,Asmir Begovic aliyesajiliwa kutoka klabu ya Stoke aliichezea Chelsea kwa mara ya kwanza dhidi ya Swansea baada ya kutolewa nje Courtois.