
Kosa lililofanywa na kipa Cech, liliwapatia West Ham bao la kuongoza katika
kipindi cha kwanza baadae tena kipa huyo aliyetokea Chelsea alipitwa na shuti dogo la Mauro Zarate na kuingia nyavuni.

Sasa Wenger hajamtupia lawama kipa wake bali anaamini uimara wa West Ham uliotokana na kushiriki ligi ya Europa ndio sababu kubwa.
Harry Redknapp "Arsenal watachukua taji wakipata mshambuliaji"
Kama alivyonukuliwa na Express amesema " Hatukua katika hali ya kulinda wala kushambulia. Nilijua mchezo ungekua ni wa mbinu, kama huwezi kushinda mchezo, hakikisha huupotezi.
"Tunajua uimara wao, West Ham walituzidi, tayari wamecheza michezo ya ushindani. Huwezi kuwafananisha na kawaida yao. Wamecheza vizuri, tutashughulikia huu udhaifu"
Liverpool yatamba, shukrani kubwa kwa Coutinho
"Leo tumeumizwa vichwa, lakini ni nafasi nzuri ya kujirekebisha" Alimaliza