Header ads

Header ads
» » Simon Msuva Akimbiza Tuzo za Lig ya Mpirai, Anyakua Mbili..Wazazi Wake Wapewa Bonge la Ofa na TFF

Simon Msuva ameibuka kidedea baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2014-2015 zilizotolewa na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na kukabidhiwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kwenye hafla iliyofanyika usiku wa leo kwenye ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF) jijini Dar es Salaam.

Msuva ambaye amechukua tuzo mbili usiku wa leo, mbali na kuwa mchezaji bora Msuva amepewa tuzo ya mfungaji bora baada ya kutupia kambani jumla ya magoli 17 kwenye msimu uliomalizika Mei 9 mwaka huu na magoli hayo yaliisaidia Yanga kuibuka mabingwa wa ligi hiyo.

Lakikini kutokana na Msuva kuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, zawadi zake zilichukuliwa na wawakilishi wake ambaye ni baba yake mzee Msuva aliye ambana na mkewe mama yake Simon Msuva.

Msuva amewabwaga Mrisho Ngassa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye kinyang’anyiro hicho cha mchezaji bora wa ligi.

Nafasi nyingine ambazo zilikuwa zikiwaniwa ni pamoja na mlinda mlango bora ambapo tuzo hiyo imenyakuliwa na Shaban Kado (Coastal union) ambaye kwa sasa amesaini kuitumikia klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwabwaga Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).

Shabani Kado akipokea tuzo yake
Shabani Kado akipokea tuzo yake

Tuzo ya kocha bora imekwenda kwa Mbwana Makata aliyekinusuru kikosi cha Tanzania Prisons kisishuke daraja. Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na Goran Kopunovic (Simba SC) pamoja na Hans Van Der Pluijm (Young Africans).

Israel Mjuni Nkongo amenyakua tuzo ya mwamuzi bora akiwabwaga Jonesia Rukyaa na Samwel Mpenzu kwenye nafasi hiyo.

Mtibwa Sugar nao wamechukua tuzo ya timu yenye nidhamu iliyokuwa ikiwaniwa na Mgambo JKT pamoja na Wekundu wa Msimbazi Simba.

Wakati Huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi, jana usiku lilitoa ofa kwa wazazi (baba na mama) wa Simon Msuva kuhudhuria mechi mbili za timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ itakapokuwa ikicheza dhidi ya Uganda kwenye michezo ya awali kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).

Malinzi ametoa ofa hiyo kwa wazazi wa Msuva ambaye jana alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara iliyomalizika Mei 9 mwaka huu ikiwa kama zawadi na shukrani kwa wazazi hao mara baada ya wazazi wa Msuva kueleza njia ndefu aliyopita mtoto wao kufikia mafanikio anayoyapata hivisasa na wao kusimama nyuma yake kwa kila jambo gumu na rahisi alilopitia kijana wao.
Viongozi wa klabu ya Yanga wakikabidhiwa mfano wa hundi ya zawadi ya bingwa wa ligi iliyomalizika yenye thamani ya shilingi miolioni 80 za Tanzania
Baba yake Simon Msuva (mzee Msuva) akiwa ameinua juu tuzo ya mfungaji bora wa ligi iliyokwenda kwa Simon Msuva, (kulia kwake) ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia na (kushoto kwake) ni mama yake Simon Msuva




 
Wazazi wa Simon Msuva wakiwa wameshika tuzo ya mtoto wao mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Mh. Juma Nkamia aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo
Shabani Kado akipokea tuzo yake ya golikipa bora wa msimu uliomalizika
Mh. Juma Nkamia (kulia) akiteta jambo na Rais wa TFF Jamal Malinzi
Mwakilishi toka Mtibwa Sugar akipokea tuzo ya timu yenye nidhamu
Mbeya City nao walipata zawadi ya mshindi wa nne
Katibu mkuu wa Yanga Jonas Tiboroha (kulia) naye alikuwepo
Mh. Juma Nkamia akitoa hotuba
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akiwa pamoja na baba yake Simon Msuva
 Mke wa Juma Nkamia ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Viajana, Utamaduni na Michezo naye alikuwepo kwenye ugawaji wa tuzo (kushoto) ni mtoto wa Naibu Waziri
Kocha wa Yanga Hans van der Pluijm jana alimwagwa kwenye kinyang'anyiro cha kocha bora wa ligi msimu uliopita na tuzo hiyo kwenda kwa Mbwana Makata
Mohamed Hussein 'Tshabalala' alikuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wakiwania tuzo ya mchezaji bora
Hizi ndio tuzo zilizokuwa zinagombewa kabla hazijaanza kukabidhiwa kwa wahusika

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post