
Hiyo ni siku chache tangu utokee mgogoro kati yake na Simba inayommiliki akidai kuwa mkataba wake umeongezwa mwaka mmoja kati ya misimu miwili aliyoisaini huku timu hiyo ikisisitiza kiungo huyo alisaini miaka mitatu.
Timu ya Azam FC ni moja kati ya klabu zinazowania saini ya kiungo huyo mwenye kasi ndani ya uwanja kwa ajili ya kumsajili katika usajili wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha timu hiyo, Haji Manara alisema kuwa wamezipata taarifa hizo za mchezaji kufanya mazungumzo na moja klabu bila ya kuihusisha klabu inayommiliki.
Manara alisema, bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina katika kuzijua klabu hizo zinazofanya mazungumzo na Messi kwa siri na endapo watazijua kwa ushahidi basi watachukua maamuzi magumu.
“Tumegundua kuwa, katika sakata hili linaloendelea kati yetu na Messi zipo baadhi za timu zinahusika katika kumshawishi mchezaji huyo kwa kulazimisha kuwa mkataba umeisha wakati siyo ukweli.“Tunaziomba hizo timu zinazomuhitaji kutufuata tu kwa ajili ya kufanya mazungumzo kama kweli zinamtaka na siyo kufanya ujanja ujanja, naomba nikwambie ukweli kuwa timu hizo zitakula wa chuya.
“Wao walete fedha tu ile tunayoihitaji sisi katika kumruhusu kama ni shilingi milioni 200 au 300 wao watoe, ninaomba watuelewe,”alisema Manara.