Mkali wa tenisi Serena Williams alimshinda Lucie Safarova seti 2 – 1 za msururu wa 6-3, 6-7 na 6-2, na kushinda taji la Roland Garros kwa mara ya tatu.
Wakati huo huo, Serena Williams ameweza kufikisha Grand Slam 20 katika mkusanyiko wake wa mataji makuu ya mashindano ya tenisi.
Serena Williams mwenye umri wa miaka 33 sasa ameweza kupiga hatua zaidi na kukaribia rekodi ya ushindi wa Grand Slam 22 inayoshikiliwa na mwanatenisi wa zamani wa Ujerumani Steffi Graf.