Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mpanda kushuhudia na kumdhamini ili apate sifa za kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Juni 15, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wanaCCM wa kijijini kwake Kibaoni wilayani Mlele Juni 15, 2015 wakati alipokwenda kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kabla ya kudhaminiwa na wana CCM wa kata hiyo katika nia yake ya kutafuta uteuzi wa CCM wa kugombea urais katika uchaguzi ujao.
Baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya wilaya ya Mpanda kumdhamini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM kugombea nafasi ya rais wa Tanzania.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wanaCCM waliofika kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kumdhamini katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya urais Juni 15, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).