Mkali wa R&B kutoka bongo anaekimbiza hivi sasa kwa ngoma yake ya Sophia Ben Paul wiki chache zilizopita baada ya kunusurika kwenye ajali ya boat hichi ndicho alichokisema
"Kabla ya safari marafiki zangu waliniambia niwapigie watu wengi simu yani rafiki zangu wafike hata kumi " 'Mimi nikawaambia nikiwaita rafiki zangu tutatumia gharama nyingi ' alisema Ben pol
"Mimi nilikuwa naangalia kwenye gharama tuu wao wantaka tuongezeke tuwe wengi, sijui wangekuja afu wakafa ingekuaje"
Kwenye ajali hiyo ya boti ambayo Ben alikua akitokea kisiwa cha mbudya ,boti ilizama yote na wao kunusurika kwa kuelea kwenye maji kwa masaa yasiopungua mawili na nusu kwa kuwa walikua na makoti ya kusaidia majini
Ben pia aliongezea kwa kusema tukio hili limemfanya apate moyo zaidi wa kuzidisha kuwasaidia watu wasiojiweza kama shukrani kwa mungu kuokoa maisha take