Header ads

Header ads
» » Facebook Yaanzisha Njia ya Kusambaza Habari za Watoto Waliopotea

 A smartphone user shows the Facebook application on his phone in the central Bosnian town of Zenica, in this file photo illustration from May 2, 2013....
Huku watumizi wa Facebook wakibuni mbinu za kusaidia kuboresha usalama kama vile vikundi vya usalama kwenye mtandao huo, kuanzia leo kuna jinsi mpya ya kuweza kusaidia kuwatafuta watoto waliopotea karibu na ulipo kwa kutumia Facebook.
Facebook itashirikiana na Kituo cha Watoto Waliopotea kilichoko marekani ili kutuma jumbe kwa watumizi wa Facebook kulingana na sehemu walioko iwapo kuna ripoti yeyote ya mtoto kupotea sehemu hio.
“Facebook, ndio mchungaji mkuu ujirani duniani,” alisema Emily Vacher, meneja wa Usalama wa Facebook wakati wa uzinduzi wa teknolojia hii mpya.
Pindi idara za usalam zitakapotoa ujumbe, Facebook itakutumia wewe ujumbe hadi kwenye simu au kompyuta yako ulio na habari kamili za mtoto aliepotea kwenye eneo lako.
“Inaweza kuwa picha ya mtoto, maelezo kuhusu gari ambayo huenda ilionekana, ama habari yoyote ambayo imefikishwa na wasamaria wema ili kusaidia kupatikana kwa mtoto aliepotea,” alisema Vacher.
Watumizi wa mtandao wa Facebook wataweza kuusambaza ujumbe huo kwa marafiki zao kwa matumaini utawafikia watu wengi zaidi.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post