Mwanamke mmoja maeneo ya Bronx mjini New York huenda akatiwa korokoroni baada ya kushtakiwa kwa kuwa mke wa wanaume 10.
Liana Barrientos, 39, alikataa mashtaka aliosomewa siku ya Ijumaa baada ya polisi kusema alidanganya katika ndoa yake ya kumi kwa kuwa na cheti cha ndoa cha 2010 kilichoonyesha hajawahi kuolewa kabla ya hapo.
Polisi walisema kwamba waligundua Barrientos alikuwa ameshaolewa mara tisa mbeleni huku ndoa zote zikisajiliwa mjini Bronx na vyeti kutolewa.
Wawili kati ya waume 10 wa Barrientos wamemfungulia mashtaka.
Makaratasi yake yote yalionyesha kwamba tisa kati ya ndoa hizo kumi zilifanyika baina ya Novemba 1999 na Agosti 2002.
Endapo Barrientos atapatikana na hatia, huenda akawekwa gerezani kwa miaka 4.