Header ads

Header ads
» » Daftari la Wapiga Kura linatarajia kuanza katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga


Zoezi la Uandikishaji  daftari la kudumu la wapiga Kura linatarajia  kuanza  katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga, zoezi litakaanza rasmi tarehe 2/06/2015 hadi 04/07/2015.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi imebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kutumia teknolojia ya BVR (Biometric Voters Registration.Vituo vya uandikishaji vitakuwa kwenye vitongoji, mitaa na Vijiji katika kata zote za mikoa hiyo iliyotajwa hapo juu  na vituo vifunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
 
Watakaohusika ni;
Waliotimiza miaka 18 na watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi oktoba 2015.
 
Waliojiandikisha  awali kwenye Daftari la kudumu la wapiga ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya.
 
Wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika kwenye vituo vilivyoko ndani ya kata zao.
 
Uandikishaji utafanyika kwa muda wa siku saba kwa kila kituo.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post