HII ni dunia ya mambo mengi! Mkazi wa Kigogo -Luhanga jijini Dar, aliyefahamika kwa jina la baba Juma, Jumamosi iliyopita alijikuta akitimuliwa ukweni sanjari na mkewe, Mwanahamisi Njama kwa madai amekuwa akishindwa kutoa ushirikiano wakati wa kuchangia chakula kwenye familia ya mkewe.
Richard Bukos, Dar

Baba Juma akitimuliwa ukweni.
Katika sakata hilo, baba Juma inasemekana amekuwa akiishi ukweni hapo
ambapo masuala ya msosi wanachangia kwa zamu na familia nzima kila
mmoja na siku yake.Kwa mujibu wa chanzo chetu, zamu ya wanafamilia
wengine ikifika hununua chakula chenye mvuto kinywani, kama samaki wa
Mwanza (sangara, sato) na mapochopocho mengine lakini zamu ya
Mwanahamisi, mumewe hutoa pesa ya matembele jambo linalodaiwa lilikuwa
likiwakera wanafamilia hao.Kufuatia kero hiyo, kwa mujibu wa chanzo, wanafamilia hao inadaiwa waliamua kumvalia njuga baba Juma na kumtimua yeye na mkewe na mtoto wao Juma mwenye miaka miwili.
Ni wakati mtafaruku huo wa ‘aondoke huyo’ ukiwa umepamba moto, chanzo chetu hicho kilipiga simu Ofisi za Global Publishers, Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kupasha mchezo kamili na akusema kuwa timbwili hilo lilikuwa likiendelea ‘laivu’....Bila kuchelewa, mmoja wa makachero wa OFM kwa kutumia pikipiki iendayo kasi, ndani ya dakika chache alifika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wanafamilia hao wakiendelea kuwafanyia timbwili Mwanahamisi na mumewe ikiwemo kuwapa vichapo huku wasamaria wema wachache wakijaribu kutuliza.
Utetezi wake ulipingwa vikali na wanafamilia hao hasa mama yao mdogo aliyefahamika kwa jina la mama Hashimu.
Baada ya varangati kuzidi, Mwanahamisi aliona ni heri ambebe mwanaye na kukimbia naye huku mumewe akimfuata kwa nyuma na kwenda kusikojulikana.
Kwa vile kisa kilisikika wakati wa mzozo, gazeti hili lilifanya jitihada za kuzungumza na wanafamilia hao ili kusikia kutoka kwao lakini ilishindikana baada ya kukosa ushirikiano kutokana na hasira za kupigwa picha.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHER