Msanii alikiba ambae hivi majuzi kwenye tuzo za KTMA aliibuka shujaa kwa kutwaa tuzo 6 wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari mapema Jana alisema
Hafurahishwi kabisa na hizi team zilizopo mtandaon kwa mashabiki wanaojiita #TeamKiba & #TeamDiamond kwani anaamini ndio zinazochochea kuonekana kati Yao wawili wana ugomvi
"Lakini ukweli ni kwamba sina ugomvi na msanii mwenzangu (diamond plutnumz) alisema Alikiba
Mbali na hapo pia mkali alikiba alichukua time yake pia kuwashauri na kuwaomba mashabiki waachane na haya mambo ya Team Team mtandaoni hasa (Instagram &Facebook) kwani ndio pekee inayoonyesha kuwa wasanii hao wapo kwenye ugomvi mkubwa lakini kumbe ni tofauti
Kiba pia aliongezea kwa kusema wao ni vioo vya jamii wanapendwa na watu wengi sana asingependa kuona mambo mabaya kati Yao yanaendelea
" kiukweli sifurahishwi na timu hizi na ni naona kinachoendelea lakini siwezi kufanya lolote kuwaingilia mashabiki ninachowashauri ni waache tu" alisema Kiba
Kwa habari nyingi nyingne endelea kubaki hapa hapa utazipata ,lakini pia mshirikishe na mwenzako azione zote hizi
.......Ahsante.....