Pamoja
na mvua hizi kulaumiwa na kulaaniwa kila kona kwa kuleta madhara pamoja
na kupoteza maisha ya watu, mvua hizi sio balaa kwa kila mtu bali kwa
wengine ni neema na zimestahili pongezi!.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadick, amezipongeza mvua
zinazoendelea kunyesha katika jiji la dar es salaam, kwa mvua hizo
kuisaidia serikali katika utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu,
kuwaamuru wakazi wa mabondeni kuhama kwa lazima, ambapo waligoma kata
kata kuhama, na serikali ilikuwa bado inajishauri namna ya kuwahamisha
watu kwa nguvu bila kuleta madhara, haswa kwa kuzingatia huu ni mwaka wa
uchaguzi!, mvua hizi zinazoendelea kunyesha zimeisaidia serikali
kuwahamisha wananchi hao, hivyo Meck Sadik amezishukuru sana!.
Mkuu
huyo wa Mkoa, ametoa shukrani hizo, katika mahojiano ya moja kwa moja
katika kipindi cha Kumepambazuka, kinachorushwa na Redio One Stereo leo asubuhi .
Amesema
ametokea taarifa za kupoteza maisha kwa watu wengine wawili, mmoja
amesombwa alipotaka kuvuka mto Ng'ombe maji yakamzidi nguvu na kumsomba,
na mwingine ni mtoto mdogo wa miaka miwili, alikuwa akicheza nje ya
nyumba yao mafuriko yakapita mbele ya nyumba na kumsomba!.
Kuhusu
wakazi wa mabondeni, Mkuu wa Mkoa alisema baada ya mafuriko ya 2011,
waliwahamisha na kuwapatia viwanja Mbweni, baadhi yao walihama na
wengine waligoma na kwenda mahakamani ambapo serikali ilizuiliwa
kuwahamisha kwa nguvu.
Hoja
za wakazi hao kupingwa kuhamishwa ni kwa sababu wametumia gharama kubwa
kwa ujenzi na kuwekewa huduma muhimu za maji na umeme, hivyo hawawezi
kuhama bila kufidiwa!. Lakini sasa mahakama imeishatoa uamuzi lazima
wahame, na serikali ilijipanga kutumia nguvu kuwahamisha, tena this time
bila kuwapatia maeneo mbadala, lakini kabla ya utekelezaji wa zoezi
hilo, Mungu akaleta mvua saidizi ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa
kuwahamisha, hivyo kuipunguzia serikali kazi ya kuwahamisha kwa nguvu.
Mkuu
wa Mkoa amesema baada ya usaidizi huu wa mvua kwenye kuwahamisha watu
hao, sasa serikali imebakiwa na kazi ndogo tuu, kuhakikisha watu hao
hawarudi katika maeneo hayo, na kuwasisitiza wale wote walohama na
kubakiza baadhi ya vifaa vyao, mvua zikisimama wataruhusiwa kivichukua
kabla ya kupitisha tingatinga na kulisawazisha eneo lote kubaki
tambarare kama walivyofanya kwa eneo la Kipawa!.
Pia
Meck Sadiki aliviomba vyombo vya habari kutoa ushirikiano katika zoezi
hili kuhakikisha wakazi wa mabondeni wanahama kwa ridhaa yao kutekeleza
amri ya mahakama na wale wote watakao kaidi, watahamishwa kwa nguvu.
Pasco.