Pazia la robo fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya limefunguliwa leo ambapo Real Madrid imekutana na mahasimu wao Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente Caldero, Spain.
Macho na masikio ya mashabiki yalikuwa upande wa mechi hii.. dakika 90 za mchezo zikakamilika kwa sare ya kutokufungana, 0-0.
Beki wa Real Madrid, Marcelo kabla ya mechi hiyo aliwaomba mashabiki wasiwe na hofu kwa kuwa kikosi chao kilikuwa kiko sawa kabisa, lakini imeonekana wapinzani wao pia walijipanga kuhakikisha hawafanyi makosa kuipoteza mechi hiyo ngumu.
Upande mwingine ilikuwa patashika kati ya vigogo wa Juventus na Monaco, dakika 90 zikakamilika pamoja na za nyongeza nyingine nne lakini Juventus walitoka kifua mbele kwa goli 1-0, ambapo Arturo Vidal alishinda goli hilo pekee kwa njia ya penalty.
Kimbembe kingine kiko leo uwanjani, Bayern Munich watakunjana na FC Porto hukuParis SG wakishikana mashati na FC Barcelona.