Bunge
limehairishwa hadi jioni baada ya vurugu kuibuka kwa baadhi ya Wabunge
wakitaka hoja ya kuhairisha mchakato wa kura ya maoni ujadiliwe maana na
kura ya maoni isogezwe mbele maana muda hautoshi na wananchi
wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Mnyika alisimama na kutoa hoja
Mnyika:
"Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge
zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima, mpaka
sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili
ni la dharura na ilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie, majibu
tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano hamna kitu"
Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza, nimesema majibu mtajibiwa baadaye
Wabunge walisimama na kupiga kelele wakitaka majibu ndipo Spika Anna Makinda akalazimika kusitisha Bunge hadi jioni.