Header ads

Header ads
» » Simulizi: SITAISAHAU TANGA | Sehemu ya Pili



 Habari wasomaji  wangu naamini muwazima wa Afya tele, Leo simulizi yetu inaendelea kama ifuatavyo...
Nikiwa chumbani nimejiinamia mara demu wangu wa Dar akanipigia simu na kuniambia kuwa nimempotezea siku hizi kwani tangu nimerudi sijaonana nae, sikutaka kuongea mengi ila nikamwambia asijari nitaonana nae tu. Wakati najiandaa kulala binti wa Kitanga naye akanipigia,
BINTI: Mpenzi ulikuwa unaongea na nani kwenye simu?
MIMI: Ni rafiki yangu wa kawaida tu mpenzi.
BINTI: Niambie ukweli tafadhari.
MIMI: Huo ndio ukweli mpenzi.
BINTI: Sawa ila nitakachofanya usinilaumu badae.
MIMI: Jamani mpenzi unataka kufanya nini tena?
BINTI: Si nilikukataza kuongea na wanawake wewe, na kwanini unanidanganya?
MIMI: Aaah samahani mpenzi, sitarudia.
Akakata simu, nikawaza sana bila ya kupata jibu nikaamua kulala tu.
Asubuhi nikashtushwa na simu yake,
BINTI: Mbona hukushusha chandarua usiku?
MIMI: Umejuaje mpenzi? Nilisahau bhana.
BINTI: Usijari mpenzi.
Basi nikaamka na kwenda zangu kuoga, nikarudi na kuvaa ili nijiandae kwenda kwenye mishe zangu. Mara simu ikaita.
BINTI: Mpenzi hiyo tisheti uliyovaa siipendi.
MIMI: (Nikiangalia ile tishirt yangu), umejuaje kama nimevaa tishirt usiyoipenda?
BINTI: Nimejua tu mpenzi, unajua mi nakupenda kwahiyo mambo mengi unayofanya yanakuja kwangu kwa hisia.
MIMI: Asante kwa upendo wako mpenzi basi nitaibadili usijari.
Nikakata simu na kwenda kwenye mishe zangu. Ila nikawaza sana kama yale mambo ni upendo kweli au kuna vitu vya ziada katikati hapa, nikaamua kupotezea na kufanya mambo mengine.
Nikarudi home nikiwa nimejichokea hata nikaona uvivu kwenda kutafuta msosi. Nilipofika nikajilaza kitandani na kujikuta nikipitiwa na usingizi hapo hapo.
Nikaanza kuota nipo sehemu nzuri sana na mchumba angu huyo wa kitanga, tukienjoy na kula raha tu.
Kulivyokucha nikaamka na kwenda kuoga kama kawaida, nakumbuka jana jioni nilikuwa na elfu themanini kwenye wallet, nikaichukua na kuicheki ile pesa nakuta imebaki elfu thelathini nikaanza kujiuliza elfu hamsini imekwenda wapi. Mara yule binti akawa anapiga simu,
BINTI: Mpenzi jana tulienjoy eeh!!
MIMI: Aaaah, eeeh wapi tena?
BINTI: Si ndotoni mpenzi!!
MIMI: Kivipi mpenzi?
BINTI: Yani ndoto uliyoota wewe usiku na mimi nimeota hivyo hivyo.
Akakata simu bado nikawa najiuliza juu ya upotevu wa pesa yangu. Mara akanitumia sms "usijari mpenzi, hiyo pesa tumeitumia ndotoni"

ITAENDELEA LAKINI NAITAJI MAONI YENU PIA KUHUSU SIMULIZI YETU IENDELEE KWA SIKU NGAPI KWA WIKI?!!
maoni yako unaweza tuma hapa hapa au kwenye ukurasa wangu wa facebook BOFYA HAPA

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post