

Kesho yake walikamatwa na wananchi walioshirikiana na polisi, baadaye kukatokea kutoelewana baada ya jeshi hilo kutaka kuwachukua ili kuwapeleka mbele ya sheria.
“Polisi waliwaweka katika gari lao ili waondoke nao, lakini wananchi waliwachomoa na kuwapa kipigo kisha kuwateketeza kwa moto, askari walijaribu hata mabomu ya kutoa machozi, lakini wakazidiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kamweli alikiri kutokea kwa tukio hilo.