Header ads

Header ads
» » Ngassa asaini Sauz



HABARI ni kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amemalizana na Klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo kusisitiza kuwa ataondoka klabuni hapo baada ya uongozi kutomlipia deni lake analodaiwa na benki.Wiki iliyopita kiungo huyo aliliambia gazeti hili kuwa yupo kwenye mazungumzo na klabu kutoka nchi za DR Congo, Qatar na Afrika Kusini.

Free State Stars inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet ipo nafasi ya 14 katika msimamo ikiwa na pointi 22 huku Kaizer Chiefs ikiongoza ikiwa na pointi 54.Mtu wa karibu na Ngassa amefichua siri hiyo na kusema tayari mchezaji huyo amemalizana na Free State Stars na mshahara wake unatajwa kuwa dola 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 8), kiwango ambacho hajawahi kulipwa kama mshahara tangu aanze soka.

“Ukweli Ngassa ana kila sababu ya kuondoka Yanga na kwenda kucheza soka la kulipwa Sauz, ni kutokana na mshahara mnono alioahidiwa kulipwa. “Dola 5,000 siyo mchezo, ukiangalia hata hao wachezaji wa kulipwa wanaocheza soka hapa nchini hakuna anayemfikia, nafikiri ni maamuzi sahihi,” alisema mtu huyo wa karibu.

Alipotafutwa Ngassa na kuulizwa juu ya suala hilo, alisema: “Kama nilivyokwambia nipo kwenye mazungumzo na klabu tatu, tuombe Mungu kama nikifanikiwa kusaini basi haraka nitakujulisha. Kiungo huyo anaendelea kulipa shilingi milioni 45 alizokopa benki kwa ajili ya kulipa deni alilokuwa anadaiwa na Simba na faini aliyopigwa na TFF baada ya kukiuka masharti ya mkataba wakati anatoka Simba kwenda Yanga.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post