Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu
kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki
kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo
yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa
kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya
kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi
unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao
wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi
kwa ulipaji kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh
Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa
matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola
milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa
tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni
tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa
yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali
Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa
majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye
mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu
nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa
na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni
900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha
21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo
Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani
ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia
40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian
inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi
kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani
ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi
la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya
dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya
dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la
makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya
rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini
anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa
Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi
milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa
kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja
Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya
maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi
bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana
wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi
kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari,
Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya
Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la
Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi
mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M
(Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo
yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia
42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado
hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini
Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality
Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na
utajiri wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika
orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa
bilionea nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha
hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya
shilingi bilioni 136 kwa mwaka