Mpaka sasa HUAWEI wameendelea kuongoza kwa kuzimiliki headlines kubwa
za dunia kutokana na bidhaa mbalimbali walizozindua ambapo leo ilikua
ni zamu ya hii saa ya kisasa.
Ni saa ambayo pamoja na mambo mengine, inakupa muda kama zilivyosaa
nyingine, simu yako inaweza kuwa mbali na wewe lakini hii saa
ikakuonyesha nani anakupigia, inakupa utabiri wa hali ya hewa, kuna
sehemu ya kukutunzia kumbukumbu za vitu unavyotaka kufanya.
Hizo ni baadhi ya sifa zake tu.
Inapatikana katika muonekano tofauti kama inavyoonekana hapa.