Header ads

Header ads
» » Katika hili Dr. Slaa amedhihirisha Tundu Lissu alikurupuka na kuna mgongano ndani ya CHADEMA



Wana jamvi mtakumbuka baada ya hukumu ya mahama kuu juu ya swala la Mh Zitto na chadema..! Tundu Lissu kwa haraka aliitisha vyombo vya habari akiwa pembeni na Godbless J Lema sambamba na Dr.W.Slaa na kutangaza kuwa Zitto si mwanachama wa Chadema!

Baada ya hilo watu wengi walikuwa na maoni tofauti juu ya hatua ya Lissu na baadhi ya wabunge wachadema walionesha kuwa Tundu Lissu alikuwa amekurupuka na si mtulivu kabisa hawa walikuwa ni Mh Mdee na Mh Wenje!

Lakini hivi karibuni Dr Slaa amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari alipo ulizwa swala la kuwaandikia barua tume ya uchaguzi ya kuthibitisha kumvua ubunge Zitto kabwe ili nao wa muandikiea Spika lakini cha kushangaza Dr Slaa alinukuliwa akisema Swala la kumvua ubunge Zitto kwao si kipaumbe bali wana mambo mengi ya kufanya!

Hapa ndio wana jamvi mnaweza kujiuliza Chadema ni chama cha namna gani? Chadema ni chama cha wakurukupaji? Ni majuzi Lissu aliulizwa swala la kuwaandikia tume ya uchaguzi barua na akasema kuwa hiyo ni kazi ya Dr Slaa lakini mtu mnaweza kujiuliza Slaa na Chadema hawakufahamu kuwa wanatakiwa kuwaandikia tume ya uchaguzi barua ya kumvua uanachama Zitto? au wanafikiri ubunge huvuliwa kwa mdomo?

Pamoja na maneno ya Dr Slaa kuonesha Lissu alikurupuka lakini tusisahau wakati Lissu anatoa tamko Slaa na Lema walikuwa pembeni hivyo alikuwa anajua anacho takiwa kufanya.

Hivi ni kama ni kweli swala la Zitto halikuwa kipaumbele kwa Chadema zile mbwembwe za kuita waandishi wa habari zilitoka wapi?Ni kweli Slaa ameshindwa kuwaandikia NEC barua? Chadema na Slaa wanaogopa na wanakwamishwa na nini?

Katika hili ni wazi kuna mvutano ndani ya chadema juu ya swala la Zitto lasivyo Slaa ange shaiandikia barua NEC maana hiyo barua haihiitaji masaa mawili!

Ni lini viongozi wa chadema wataacha kukurupuka?wana tofauti gani na futuhi?

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post