
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa msaada wa mabati 850 ikiwa ni ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kusaidia waathirika wa mafuriko katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama.Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa (pichani), alisema msaada huo una thamani ya Sh. milioni 12.Dk. Slaa alifafanua kuwa kati ya kiasi hicho cha fedha zilizonunua mabati, Sh. milioni 10 ni sehemu ya ruzuku inayotolewa na serikali kwa chama hicho na kiasi kingine ni michango iliyopatikana katika mikutano ya hadhara ya chama hicho iliyofanyika mjini Kahama.Alisema waliamua kununua mabati hayo kutokana na kamati ya mkoa inayoratibu maafa hayo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga, kupendekeza vinunuliwe vifaa vya ujenzi kutokana na chakula kuwapo cha kutosha.
Dk. Slaa aliwataka viongozi kuhakikisha wanasimamia vema ujenzi wa nyumba za kuduma za makazi ya wananchi wa kata ya Mwakata kama ilivyopendekezwa na Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea waathirika hao kwani mara nyingi serikali imekuwa ikishindwa kutekeleza kwa wakati majanga kama hayo.“Niwaombe viongozi wa mkoa kusimamia waathirika hawa wajengewe nyumba kwamuda mwafaka…
Watanzania wengi tanawakatisha tamaa kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zinazotolewa kama kule Kilosa hadi leo bado watu wanaishi kwenye mahema, tangu nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, naomba sana Shinyanga muwe wamfano,” alisema Dk. Slaa.
Katika hatua nyingine, misaada imeendelea kutolewa kwa waathirika hao baada ya Kampuni ya Simu (TTCL), kutoa chakula na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. milioni tatu.Meneja wa TTCL Mkoa wa Shinyanga, Peter Kuguru, alisema kampuni yake imeungana na Watanzania wengine walioguswa na maafa hayo kutoa msaadawa kibinadamu na kuyaasa mashirika mengine na watu mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wananchi hao.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- Unknown
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Matumizi mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija, kampuni moja ya te...
-
Teknolojia imetuondoa katika mazingira yaliyokuwa yakituzunguka na kutupeleka katika mazingira ambayo si halisi, tuna marafiki wengi w...
-
MATUKIO ya ukatili wa kutisha yanazidi kushika kasi kila kona ya nchi, safari hii h...
-
Mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua nyumba 4 kwa ajili ya kuzibomoa na kujenga upya katika eneo la Palo Alto lililok...
-
Inawezekana labda umesha-wahi kuisikia au kuiona ila kwa faida ya wale ambao hawajawai kuiona wala kuisikia ni kwamba computer stick ni...
-
Mchezaji bora duniani wa soka Lionel Messi , ameteuliwa kuwa balozi wa kimataifa wa kuwakilisha kampuni ya Huawei . Msimamizi mkuu wa H...
-
Kampuni ya Google imetambulika kuwa bidhaa yenye thamani zaidi kwa mujibu wa shirika la fedha la linalojihusisha na ukaguzi wa thamani ya...
-
Nchini Sudan Kusini mara kwa mara imetambulishwa kwa kuwa eneo la vita ,mauaji na ghasia,sasa matumaini yameanza kupnekana baada ya rai...
-
Kifaa kinachotambulika kwa jina la OralQuick kilichoundwa nchini Marekani sasa chaweza kutumika katika kupima virusi vya UKIMWI kwa ku...
-
Utafiti mpya wa Taasisi ya Taaluma za Teknolojia ya Japan (NII) unazua mashaka juu ya pozi hili maarufu la kupigia picha, hasa miongon...
Data Boosta