Sasa ongezeko la bei za sare na vifaa vya shule linalofanywa na wafanyabiashara sehemu mbalimbali hapa nchini, limewaweka wazazi njiapanda.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa sehemu mbalimbai hasa kwenye maduka ya vifaa vya ofisini katika sehemu nyingi hapa nchini, bei ya sare za shule za msingi na sekondari, madaftari, vitabu na
vifaa vingine zimepanda mara mbili ya bei iliyokuwa mwaka jana.
Na hii imeshakuwa desturi kwa wafanyabiashara wengi unapofika wakati wa kufungua Shule ndipo wanaanza kupandisha bei ya vifaa vya Sule, Sijafahamu ni kwa sababu gani? Kwa mfano mwaka jana bei ya begi la kubebea madaftari lilikuwa
likiuzwa Sh10,000, lakini hivi sasa ni Sh20,000.
jozi ya viatu imepanda mara tatu, kwani
mwaka jana ilikuwa ikiuzwa kwa Sh5,000 na sasa wananunua kwa Sh15,000
huku bei ya shati, sketi na kaptula ilikuwa Sh4,500 na sasa wanauziwa
kwa Sh6,500 mpaka 7,000. hii ni kwa baadhi ya sehemu hapa nchini.
Lakini baadhi ya wafanyabiashara walisema kupanda kwa bei
hizo kunatokana na bei za bidhaa hizo kupandishwa katika maduka ya
jumla wanakonunua.
“Jola la kitambaa tulilokuwa tunauziwa kwa
Sh70,000 hivi sasa tunauziwa kwa Sh120,000, hii ni tofauti kubwa, kwa
hiyo hatuwezi kuuza kwa bei ya zamani, lazima tuendane na ununuzi wa
jumla ili tupate faida kidogo,” alisema mfanyabiashara mmoja ambaye
hakutaka jina lake litajwe.
“Hatupendi kupandisha bei, hata sisi tunazidiwa na
hatuwezi kufanya biashara kwa hasara tunaenda na soko, kwa hiyo hata
wazazi nao wakubali kwenda na mabadiliko hayo ya bei,” alisema.
Wazazi hao wameiomba Serikali ione namna ya kudhibiti upandaji wa bei hizo.
Lakini kaa ujifahamu kwamba kuna wazazi wana watoto zaidi sita na wote wanahitaji kwenda
shule, na ukizingatia kipato chao ni cha kubangaiza, Je wataweza kuhimili bei hizi zinazopanda kiolela ususani mwezi huu wa kwanza, Kwa mwendo huu watoto watapelekwa shule kweli?,
Wazazi wanaiomba Serikali kudhibiti upandishwa holela wa bei za vifaa vya shule msimu huu.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Soma na Hizi
Matukio yaliyojili katika ulimwengu wa Teknolojioa Mwaka 2016
MWAKA 2016 umefika ukingoni, kwanizimesalia saa chache kabla ya kuingia 2017. Ahsante kwa...Read more »
31Dec2016TCRA imeziagiza kampuni za simu kutenganisha vifurushi
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeziagiza kampuni za simu kuanzisha vifurushi vinavyote...Read more »
02Oct2015Facebook na UN washirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet kwa wakimbizi wa Syria
Facebook na UN yashirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet katika k...Read more »
01Oct2015Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji
Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji milion...Read more »
01Oct2015Umoja wa Ulaya na China kushirikiana katika utafiti wa 5G
Umoja wa Ulaya unasema kuwa ushirikiano huu utaongezea vituo v...Read more »
01Oct2015shule zote za Serikali kufungwa nchini Kenya
Serikali yatoa agizo la kwa shule zote kufuatia mgomo wa walimu...Read more »
20Sep2015

Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Mambo vipi Rafiki yangu? Kama wewe ni miongoni mwa...
-
Nabii Samwel Mahela wa Kanisa la...
-
Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu...
-
Si wengi wetu wanaofahamu umuhimu wa kula samaki mara...
-
wakati huku kwetu bado wanafunzi wanaendeleza njia...
-
Kwa wale Rafiki zangu wa ma-gadgets and all...
-
The American Idol judge wore this eye popping red dress...
Data Boosta
